School News 21 September 2026 Admissions

Fomu za kujiunga 2027 (Nursery–Darasa la VII) zinapatikana shuleni 05–30/10/2026 kwa TSh 10,000/=.

Pupils and staff gathered in front of the administration block.

Story

Uongozi wa Shule ya St. Charles Borromeo unawatangazia wazazi na walezi kwamba fomu za kujiunga na masomo kwa mwaka 2027 zimeanza kutolewa.

Fomu zinahusu: Nursery (watoto wa miaka mitatu), Chekechea (L.K.G), Awali (U.K.G), na Darasa la Kwanza hadi la Saba.

Fomu zinapatikana shuleni kuanzia tarehe 05/10/2026 hadi tarehe 30/10/2026 kwa gharama ya shilingi 10,000/= tu.

Tarehe 10/11/2026 ni siku ya mwisho kurudisha fomu kwa wale wote waliochukua. Muda wa kurudisha ni kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.

Karibuni sana! — Sr. Anita Pinto, Mwalimu Mkuu